Facebook Comments Box

Tuesday, June 25, 2013

TAARIFA YA UHAMAJI WA OFISI ZA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.

Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.

Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013.

Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.

Simu: +255 22 2669036/2669037
Faksi: +255 22 2669039
Barua pepe: info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU