Facebook Comments Box

Monday, February 25, 2013

TAASISI YA AL JAZIRA ISLAMIC CENTRE KULIBURUZA GAZETI LA MTANZANIA MAHAKAMANI


Shekh Jabir Katula ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa kituo cha Aljazira Islamic akizungumza na waandishi wa habari huku akishuhudiwa na baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.
Uongozi wa Taasisis ya Al Jazira Aslamic Centre umekanusha habari ilizotaja kuwa ni za uongo, uzushi na ufitini zilizochapishwa na gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 13 februari 2013 na toleo la tarehe 20 februari 2013 zikikitaja kituo hicho kufadhiliwa na makundi ya Al-Qaeda na Al-Shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.

Aidha kituo hicho kimesikitishwa na taarifa hizo na kutia mkazo kulitaka gazeti hilo (Mtanzania) kuomba radhi kabla ya siku saba kutokana na demand note waliyoitoa, kinyume na hapo taasisi hiyo imesema kuwa itachukuwa hatua zaidi za kisheria.
Kusanyiko lililofika kushuhudia tamko.

Shekhe Mohamed Salum Mbala Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza.
"Habari iliyotangazwa imetustusha sana imetudhalilisha, imetuudhi ni taarifa ambayo haikufanyiwa utafiti, imevunja heshima ya waislamu sio wa Mwanza Tanzania pekee bali dunia nzima, tunasema wazi kuwa sisi waislamu tunapenda amani na tuko kwa ajili ya kuitangaza amani na hatuko tayari kuvurugwa kuipoteza amani ya nchi hii"

"Kwa kweli tunalaani sana udhalilishaji huu tunaomba mwandishi wa habari hizo atoe ushahidi na hatutokubali kama hatotoa ushahidi"
Shekhe Musa Kunenge ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre Ukerewe amesema kuwa chuo chake kilipata idhini ya waislamu kwenye msikiti, kisha kikafuata njia zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kupata kiwanja hatimaye usajili na shughuli zote zinatendeka kwa haki na uhalali na wala kituo hicho hakijihusishi na yale yanayotajwa kwenye magazeti kukichafua chuo hicho. 


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU