Mdahalo wa mwisho wa wagombea wa uchaguzi nchini Kwenya unafanyika jioni ya leo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mgombea wa Urais
Uhuru Kenyatta alikuwa amesusia mdahalo huo akidai kuwa mdahalo wa
kwanza waliokuwa wanauendesha mjadala wenyewe waliangazia sana swala la
ICC na kuwafanya wagombea wengine kumlemea.Wagombea wengine akiwemo waziri mkuu Raila Odinga wanajiandaa kwa mjadala huo ambaop hii leo utalipa kipao mbele mbele swala la ardhi, sera za kigeni, na uchumi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa asilimia tisini ya wapiga kura wanaona mjadala huu una manufaa kwa wakenya. Asilimia themanini na tano walisema wako trayari kutazama mjadala huo.
Asilimia robaini ya wapiga kura waliohojiwa punde baada ya mjadala wa kwanza walisema wangempigia kura Uhuru Kenyatta wakati asilimia 33 walisema wangempigia kura Raila Odinga.Wawili hao ndio wagombea wakuu katika uchaguzi huu.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog