WAKATI Mkutano Mkuu wa Nane wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM)
ukimalizika, mmoja wa wagombea wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
chama hicho nafasi sita Tanzania Bara, Stanley Mdoe, ametiwa mbaroni na
Polisi akibainika kuwa askari Polisi.
Askari
huyo mwenye namba F 7961 wa cheo cha Konstebo, anatoka kituo cha Polisi
Mvomero, Morogoro ambaye alibainika jana akijihusisha na siasa hata
kuingia kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC kupitia Vijana.
Kwa
mujibu wa habari zilizopatikana Morogoro, askari huyo alijitambulisha
kwa baadhi ya wajumbe kuwa yeye ni mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
Joel Bendera, akijiita Stanley Bendera.
Wapambe
waliofuatana naye kutoka Morogoro wakiwa Dodoma waliarifu kuwa mgombea
huyo alikamatwa juzi jioni akiwa amevalia sare za chama hicho akiomba
kura kwa wajumbe ili wamchague kwa nafasi hiyo.
Hata
hivyo, ilielezwa na baadhi ya wanachama waliofuatana naye na wengine
wanaotambua kazi yake uaskari, waliwajulisha maofisa usalama waliokuwa
eneo hilo nao kufikisha taarifa hizo Polisi na kukamatwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, askari huyo alikuwa ameomba likizo isiyo na malipo, wakati wengine wakidai kuwa ameacha kazi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile akizungumzia tukio
hilo alisema alipata taarifa ya kukamatwa kwa askari huyo Dodoma na
kwamba wakati huo alikuwa akimtafuta kwa siku mbili kwa ajili ya
shughuli za kikazi bila mafanikio.
“Sina
uhakika kama askari huyu amejiingiza katika siasa ... nimetuma askari
wengine kwenda Dodoma kufanya uchunguzi wa suala hilo,” alisema Kamanda
Shilogile na kuongeza:
“Iwapo
itabainika kuwa kweli, atachukuliwa hatua stahiki na kinidhamu
kulingana na taratibu za kijeshi. Hata hivyo siwezi kuzungumzia suala la
ugombeaji wake, sijathibitisha ukweli wake, isipokuwa hakuwa kazini kwa
siku mbili na ni utovu wa nidhamu kwa Jeshi letu kutoonekana eneo la
kazi,” alisema Kamanda Shilogile.
Kwa
mujibu wa Kamanda, sheria za nchi na Katiba kuna vifungu vinavyohusu
majeshi ya ulinzi na usalama vikitamka kuzuia na kupiga marufuku
mwanajeshi kujihusisha na siasa.
Alisema
iwapo jambo hilo litabainika, litakuwa limefanyika kinyume na kanuni na
taratibu za kazi ya uaskari. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bendera,
hakupatikana ofisini kwake wala kwa njia ya simu ya mkononi ili
kufafanua kadhia hiyo.
Hata hivyo wasaidizi wake walidai kuwa yuko nje ya nchi kwa shughuli za kikazi.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kusimamia na Kuendesha Upatu (DECI), Mchungaji Jackson
Mtares amekiri kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliwakataza kupokea
fedha kutoka kwa mwanachama yeyote wa taaasisi hiyo.
Mtares alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kuendesha shughuli za upatu bila kibali inayomkabili pamoja na wakurugenzi wenzake wanne.
Akihojiwa na Wakili wa Serikali Prosper Mwangamila, Mtares alidai katika barua ya majibu ya kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi hiyo, BOT iliwatakaza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote iwe kwa hiari au kwa lazima.
Hata hivyo alipoendelea kuhojiwa na kupewa barua hiyo ambayo imepokelewa mahakamani hapo kama kielelezo cha upande wa mashitaka, Mtares alidai kuwa Mkurugenzi mwenziye ambaye pia ni mshitakiwa ndiye atakayetoa maelezo zaidi.
Awali Mtares aliwasilisha kielelezo ambacho ni barua ya maombi waliyoandika kwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi ambazo ni kusaidia watu wenye kipato cha chini kujikimu kimaisha.
Akiongozwa na Wakili wake wa utetezi Hudson Ndusyepo, Mtares alidai hakuhusika kupokea fedha wala kutoa risiti kwa wanachama na hata katika ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashitaka hakuna shahidi aliyedai yeye alipokea fedha.
Mtares aliendelea kudai kuwa, Benki ya Afrika (BOA) ilikataa kuhifadhi fedha za taasisi hiyo hivyo walizihamishia katika akaunti ya kanisa lake la Jesus Christ deliverance iliyopo katika Benki ya Wananchi Dar es salaam (DCB) ambayo ilikutwa na zaidi ya Sh bilioni 1.3 baada ya shughuli za Deci kusimama.
Alipoulizwa sababu za benki hiyo kukataa kuhifadhi fedha hizo alidai hajui bali walipewa taarifa kuwa wanatakiwa watoe fedha hizo haraka ndipo bodi ya wakurugenzi ilipoamua fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti ya kanisa lake.
Aliendelea kudai kuwa wanachama walikuwa wanalipa kiingilio cha Sh 30,000 na baadaye wanaweka fedha na kupata uwezeshwaji (riba) ya asilimia 150 ya fedha ambayo mwanachama ameweka.
Alipobanwa kwa maswali na upande wa mashitaka, Mtares alidai fedha za riba zilitokana na fedha walizokuwa wanaweka wanachama kwasababu Deci ilikuwa haijishughulishi na biashara yeyote zaidi ya kuwasaidia watu wenye kipato cha chini.
Hakimu Stewart Sanga aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8 mwaka huu, wakatakapoendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Wachungaji wa makanisa tofauti ya Pentecoste ni, Dominic Kigendi, Samuel Mtares, Timotheo Ole Loitingye na Arbogast Francis.
Wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2007 na Machi 2009 katika Makao Makuu ya Deci, Mabibo Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa, katika mpango huo waliouita kupanda na kuvuna pia walifanya shughuli hiyo bila leseni.