Facebook Comments Box

Friday, August 22, 2014

YABAINIKA KAVUMBAGU WA AZAM ANATUMIA VIDONGE

Kavumbagu
Straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu ameweka wazi kuwa, anatumia vidonge maalum kuongeza virutubisho vya mwili ambavyo vinamsaidia kuwa mwepesi na kumudu programu za kocha wake.

Kavumbagu ambaye alikipiga Yanga misimu miwili kwa mafanikio aliyasema hayo hivi karibuni ambapo alikiri kuwa vidonge hivyo vinaongeza virutubisho muhimu mwilini, pia kuulainisha mwili kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi magumu ya kimichezo na si vinginevyo.

“Nimefanya vizuri katika mazoezi kwa kuwa ninapata muda mwingi wa kupumzika na kula chakula katika muda mwafaka, pia kuna rafiki.yangu yupo Ulaya amenitumia vidonge fulani vya vitamin ambavyo nikimeza vinaufanya mwili uwe huru na kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi." 

"Ni vidonge vya kawaida ambavyo mwanamichezo yeyote anaweza kutumia bila ya kupata madhara, hata Didier Drogba wa Chelsea anavitumia sana,” alisema Kavumbagu.

Alipotafutwa Daktari wa Azam, Mwanandi Mwankenwa juu ya ufafanuzi wa vidonge hivyo, alisema: 
“Navifahamu vidonge hivyo, vinatumiwa na wachezaji wengi wa Azam, siyo yeye tu, hata (John) Bocco na wengine pia wanatumia, havina madhara kiafya.”

Chanzo: champion


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU