Facebook Comments Box

Tuesday, October 1, 2013

SABABU YA CHUJI KUWEKWA BENCHI NA BRANDIS YAWEKWA HADHARANI





Athumani Idd Chuji - Kiungo mpigaji wa pasi ndefu Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts amewataka wachezaji wake wacheze pasi fupi zenye akili kwa sababu ndiyo ushindi wao na si ndefu kama wanapopoa maembe mtini na akaweka wazi kuwa, alimtumia kiungo wake mkongwe, Athuman Idd ‘Chuji’ kama mchezaji wa akiba kwa sababu hajafanya mazoezi na timu kwa muda mrefu.
Chuji aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo na dakika chache baadaye Yanga ikapata bao la ushindi lililofungwa na Hamis Kiiza raia wa Uganda matokeo yakawa ya ushindi wa bao 1-0 mwishoni mwa wiki.
Kutokana na kitendo hicho mashabiki wa soka walihoji na kupiga kelele kulikoni kiungo huyo aachwe nje wakati ni msaada kwenye timu.
Brandts alisema: “Nataka timu icheze mpira kwa pasi fupi fupi na kwa umakini na si ndefu zisizo na mpango kwa sababu ndiyo zinatugharimu na hata mechi yetu na Ruvu kipindi cha kwanza hatukuwa vizuri.” 

Akimzungumzia Chuji, kocha huyo alisema: “Sikuweza kumtumia kipindi cha kwanza kwa sababu hakuwa na muda mzuri wa pamoja na wenzake katika mazoezi na alikuwa kwao, kulikuwa na matatizo ya kifamilia.
Hali hiyo ndiyo ilinifanya nisimpange kikosi cha kwanza na ndiyo maana nilimtumia kipindi cha pili.”
Chanzo:Mwanaspoti


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU