MABAO mawili ya Mesut Ozil na Olivier 
Giroud yameipa Arsenal ushindi wa 2-0 nyumbani katika mchezo wa Ligi ya 
Mabingwa Ulaya  dhidi ya Napoli Uwanja wa Emirates. 
Ozil alifunga bao safi dakika ya nane 
akimtungua kipa hodari wa zamani wa Liverpool Pepe Reina, hilo likiwa bao lake la kwanza tangu 
ajiunge na timu hiyo kutoka Real Madrid kabla ya Olivier Giroud kufunga la pili dakika ya 15.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, 
Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Arteta, Ramsey/Monreal 
dk88, Ozil, Rosicky/Wilshere dk63 na Giroud.
Napoli:
 Reina, Mesto, Albiol/Fernandez dk83, Britos, Zuniga, Behrami, Inler, 
Callejon/Zapata dk77, Hamsik, Insigne, Pandev/Mertens dk61.


Oliver Giroud akishangilia bao lake

Ozilakipokea pasi kiustadi na kuelekea langoni mwa Napoli


Wenger na Rafa Benitez wakisalimiana 

Hasira za mashabiki wa Napoli

Ozil akiwachambua Napoli kama karanga
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog