ZACHARIA GINDU(ALIVYOJILIPUA) Na Daniel Makaka
Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na moto.
Mkazi wa kitongoji cha Kijiweni kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza, amefariki dunia baada yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki dunia akiwa ndani ya nyumba yake.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw. Juma Mashauri, amemtaja aliyekumbwa na mauti hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36) mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya Busega  Mkoa wa Simiyu.


Bw. Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo inaelezwa kuwa ni kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake na mke wake aliyetajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha Ngoma ‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo hazieleweki kuwa ni za nani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana katika ndoa yao iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vilivyosababisha mmoja  wa wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi ya kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
 
Kutokana na tukio hilo kwa upande wake  Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia tukio hilo amewaomba vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala la ulevi unaosababisha kuchukua maamuzi ya kujiua wakati Taifa bado linawategemea .
 
Naye diwani wa kata hiyo Robert Madaha amesikitishwa kwa kutokea kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha unywaji wa pombe ambao hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.