Facebook Comments Box

Wednesday, October 2, 2013

SEREKALI YAIJIBU YANGA KUHUSU MAOMBI YA UJENZI WA UWANJA

Siku moja baada ya uongozi wa Yanga kudai serikali imechelewesha majibu ya maombi ya kuongezewa eneo la ardhi, umetakiwa kwenda kuhakiki deni la kodi ya ardhi sh milioni 100 unazodaiwa tangu mwaka 1997, gazeti la Tanzania Daima limeripoti.
Yanga kupitia mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Uwanja, Francis Kifukwe, juzi ilitangaza kuwa wizara pamoja na manispaa ya Ilala zimechangia kukwamishwa kwa ujenzi wa uwanja wao unaotarajiwa kuitwa ‘Jangwani City’.

Taarifa ya Ujenzi wa Uwanja wa Yanga.
Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima, msemaji wa wizara hiyo, Rehema Isango, alisema, wao hawawazuii Yanga kuendelea kufuatilia hati katika wizara yao, bali wanatakiwa kulipa na deni hilo ambalo ni kodi ya umiliki halali wa eneo lao la Jangwani, yaliko makao makuu ya klabu hiyo inayoendesha kazi zake za kila siku.
“Yanga wao wameomba kwetu hati, na hilo haliwazuii kuendelea na mchakato huo ila cha muhimu waje waangalie kodi hiyo na wailipe,” alisema Rehema.
Msemaji huyo aliongeza kuwa jana waliwasiliana na Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, na kumweleza juu ya deni hilo na kuwataka kwenda wizarani kujiridhisha na kisha kulilipa.
Aidha Rehema alisema manispaa ya Ilala ina mpango wa muda mrefu wa kulitumia eneo hilo kwa shughuli mbalimbali na sio ujenzi kutokana na kuwa bonde.
Aliongeza kuwa Yanga kupata au kutopata eneo hilo kutatokana na maamuzi ya manispaa ambao ndio watendaji wao wakubwa.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU