Mshambuliaji wa Simba Betram
Mwombeki akichuana na mlinzi wa Mgambo JKT Bakari Mtama wakati wa
mchezo wa ligi kuu baina ya timu hizo uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam hapo jana. Matokeo ya mchezo huo ni kama yanavyoonekana katika
picha ya ubao wa matangazo hapo chini .
Timu ya Simba ya
Dar es Salaam jana katika Uwanja wa Taifa imedhihirisha umwamba wake mbele ya Mgambo Shooting
inayomilikiwa na JKT kwa kuicharaza mikwaju 6 - 0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Soka Tanzania bara. .
Magoli ya
Simba yaliyo fungwa na Hamis Tambwe aliyefunga goli 4 na Haruna Chanongo goli 2
yameiwezesha Simba kushika usukani wa Ligi kwa kuishusha hadi nafasi ya pili timu ya JKT Ruvu ambayo imecharazwa bakora 1 na Ruvu
Shooting, bao la Ruvu liliwekwa kimiani na Cosmas Nyalusi "Baloteli".
Wakati
Simba ikishangilia karamu hiyo ya Magoli imekuwa ni Mwiba kwa mahasimu wao Yanga ambapo wametoka sare kwa mara nyingine tena na Prisons "Wajelajela" baada ya kutoshana nao nguvu kwa bao 1 - 1.
Yanga ikiwa bado na kumbukumbu ya kutoka sare mchezo wao na Watoto wa Mbeya Mjini "Mbeya City"ndiyo waliokuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Gerry Tegete kwa kifua baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Prisons.
Ndani ya Chamazi Complex kama wanavyouita uwanja wao Azam FC nao wamepigwa na bumbuazi baada ya Ice-Cream zao kuyeyushwa na watoto
wa mjini Ashanti United kwa sare ya 1-1. Wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Kipre Herman Chetche wa Azam na Anthony Matangalu wa Ashanti.
Huko Kwa
wakata Miwa wa Kagera, ndani ya Kaitaba Bukoba, Kagera Sugar wamepata ushindi wao wakwanza baada ya kuifunga JKT Oljoro kwa bao 2 - 1, wafungaji wa mabao hayo ni Geofrey Aswile na Malegesi Mwangwa wa Kagera na Godfrey Nayopa wa Oljoro.
Mchezo
mwigine ulio shuhudia sare ni ule wa Wakata Miwa wa Turiani Mtibwa Sugar
iliyo toka sare ya bila kufungana na watoto wa Mbeya City.
Wagosi wa
Kaya Coastal Union ya Tanga nayo imekutana na "wajeda" kutoka Tabora, Rhino
Rangers na kutoka sare ya 1-1 wakiwa Mkwakwani.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog