Facebook Comments Box

Wednesday, September 18, 2013

KASEJA AJIUNGA NA ASHANTI AKITOKEA NDANDA FC YA DARAJA LA KWANZA

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Juma Kaseja amejiunga na timu ya Ashanti United ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akitokea timu ya Ndanda FC inayocheza daraja la kwanza kama  kocha wa makipa wao na anatarajiwa kuanza kuichezea rasmi Januari mwakani, baada ya kuchelewa dirisha la usajili.
Kocha wa makipa wa timu hiyo ya Ilala, Dar es Salaam, Iddi Pazi ‘Father’ amesema jana kwamba Kaseja amejiunga na Ashanti United na amekwishaanza kazi.
Father, alisema kwamba pamoja na Kaseja, pia Ashanti imempata kipa mwingine mzoefu, Amani Simba SC ambaye naye amekwishaanza mazoezi.
“Nipo na Amani Simba na Juma Kaseja hapa Ashanti, naamini wote ni makipa wazuri na watachuana ili kurejea matawi ya juu. Nitawafanyia kazi na watakuwa makipa bora tena,”alisema Pazi, baba wa mshambuliaji wa Simba SC, Zahor Pazi.
Kaseja aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2003 alipojiunga nayo akitokea Moro United.
Baada ya hapo, alipata ofa ya kwenda St. Eloi Lupopo ya DRC, lakini wakashindwa kuafikiana na kuamua kuangalia ustaarabu mwingine. Wakati wa maandalizi ya msimu mpya, Kaseja alikuwa akifanya mazoezi na Mtibwa Sugar iliyokuwa imeweka kambi Dar es Salaam.
Juhudi za kumpata Kaseja mwenyewe kuthibitisha kujiunga kwake na Ashanti hazikuweza kufanikiwa mapema.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU