Facebook Comments Box

Thursday, September 19, 2013

JESHI LA POLISI KUFANYA OPERESHENI MAALUMU KATIKA MAKUTANO YA BARABARA ZOTE ZA DAR


Kamanda Kova

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza operesheni maalum ya kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara katika makutano yote ya barabara kuu jijini Dar es salaam kutokana na kuwa kikwazo kiusalama wakati wa kupambana na wahalifu.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es saalam DCP Suleiman Kova amesema uwepo wa watu wasiokuwa na shughuli maalum pembezoni mwa barabara katika makutano mbalimbali jijini kumekuwa kukikwamisha askari kutekeleza wajibu wao kama ipasavyo hasa vinapotokea vitendo vya uhalifu. 

Akizungumza jijini Dar es salaam baada ya kuwatunukia Nishani maofisa wa polisi waliotumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 35 kwa kanda maalum ya Dar es salaam Kamishana Kova amesema dhamira ya jeshi hilo ni kuacha wazi makutano yote ya barabara na kudhibiti uhalifu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick amesema zoezi hilo la kuwaondoa ombaomba ni endelevu na linalenga kuliweka jiji la Dar es salaam katika hali ya usafi.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU