Facebook Comments Box

Tuesday, February 5, 2013

NDUGU WAWILI WAUWAWA KINYAMA ARUSHA






WANAWAKE wawili wanandugu wameuawa kinyama katika nyumba waliokuwa
wakiishi na watu wasiojulikana na miili yao kukutwa baada ya siku tatu
ikiwa imelaliana huku ikiwa imeharibika vibaya.
Kugundulika kwa miili hiyo kumetokea leo majira ya saa 3.15 katika
eneo la daraja mbili manipsaa ya jiji ya Arusha baada ya majirani
kuhisi harufu kali iliyokuwa ikitokea ndani ya chumba hicho
walichokuwa wamepanga katika nyumba inayomilikiwa na merehemu Samson
Kivuyo.
Taarifa zimeeleza kuwa majirani hao walijikusanya na kutoa taarifa
kwa uongozi wa eneo hilo ambao kwa pamoja walikubaliana kutoa taarifa
polisi ambapo ,polisi walifika eneo la tukio na kuvunja mlango ,ndipo
walipokuta miili ya marehemu hao ikiwa imeharibika vibaya.
Miiili ya marehemu hao ilikutwa na majeraha sehemu mbalimbali za
mwili, huku ndani ya chumba hicho kukiwa kimevurugika na baadhi ya
vitu kuvunjika hali ambayo inaaminika kwamba kabla ya mauaji hayo
kulikuwa na mvutano wa kutoelewana.
Akizungumza na vyombo vya habari msimamizi wa nyumba hiyo,Fatina
Mringo aliwataja marehemu hao kuwa ni,Zainabu Iddy(Zai) mwenye umri wa
miaka 19 na Zena Sadick Shengwatu mwenye umri wa miaka 40 ambaye
alikuwa mfanyabiashara wa nguo na mmiliki wa chumba hicho.
Alieleza kuwa siku ya jumamosi marehemu hao walionekana majira ya
mchana wakiwa nyumbani, na marehemu Zena alikabidhiwa fedha na
wapangaji wenzake na kwenda kulipia bili ya umeme Tanesco na baadae
alirudi na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Hata hivyo habari zimedai kwamba marehemu hao kwa pamoja hawakuweza
kuonekana tena hadi miili yao ilipokutwa chumbani ikiwa imeharibika
vibaya na kutoa harufu kali.
Hata hivyo baadhi ya majirani wakielezea tukio hilo wamebainisha
kwamba marehemu hao mara nyingi walionekana kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na wanaume tofauti na kwamba siku ya tukio Zena alionekana
akichukuliwa na gari dogo aina ya teksi huku gari jingine lilionekana
likingia nyumbani kwake.
Majirani hao wamedai kwamba marehemu hao ambao ni wakazi wa Lushoto
mkoani Tanga waliishi katika nyumba hiyo katika mazingira ya kutokuwa
na waume .
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi unaendelea na kwamba hadi
sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na miili ya marehemu
hao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru kwa uchunguzi wa
daktari.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU