Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa
Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya kimeridhia kusitishwa kwa Mkataba
wa Mkandarasi M/S Kalyango Contructoins And Building Company Limited
aliyekuwa akijenga daraja Nkwasi Wilayani Uvinza.
Mkandarasi
Kalyango Construction alikabidhiwa eneo la kazi Julai 5, 2012 na
kutakiwa kukamilisha ujezi wa daraja la NKWASI Okitoba 15, 2012,
lakini pamoja na kuongezewa muda hadi Desemba 30, 2012 mkarandasi huyo
alishindwa kukamilisha kazi hiyo.
Hadi
anasimamishwa mkarandasi huyo alikuwa amelipwa zaidi ya milioni 25.7
ambazo ni kati ya shilingi milioni 97.4 alizostahili kulipwa kama
angekamilisha ujenzi.
Baada
ya taarifa ya mkuu wa mkoa safari ikawa ni kuelekea eneo la ujenzi
ambapo meneja wa wakala wa barabara mkoani Kigoma Narisi Choma ndiye
aliyetoa taarifa kwa wafanyakazi wa mkarandasi Kalyango kuwa hawatakiwi
kuendelea na kazi.
Muda
na kwa nyakati tofauti wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, katika
ziara zao, wamekuwa wakiwaonya wakandarasi wanaofanyakazi chini ya
kiwango, kauli ambazo zinaungwa mkono na wakazi wa mwambao wa kusini mwa
ziwa Tanganyika.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog