Facebook Comments Box

Friday, January 25, 2013

BREAKING NEWS: MABOMU YARINDIMA DUMILA SASA HIVI



Katika hali iliyodumu muda mrefu sana ya mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Kilosa imechukua hatua mpya. Sasa hivi kuna vurugu kubwa kati ya wakulima na wafugaji ambapo hadi gari la mkuu wa wilaya limechomwa moto. Muhabarishaji wetu kutoka eneo hilo anasema kuwa hali ilifikia hivyo baada ya mkuu wa wilaya kuhalalisha mashamba ya wakulima kuwa kijiji cha wafugaji. Mpaka sasa polisi wa kuzuia ghasia wapo eneo hilo wakipiga mabomu.

Hali ya usafiri imekuwa tete kutokana na ghasia hizo. Mahakama iliamua suala hilo lipelekwe kwenye utawala na mkuu wa wilaya siku ya jumatano kaamua Mabogile kiwe kijiji hali hiyo ndio iliyoleta vurugu zote. Mkuu wa wilaya alipopigiwa kutoa maelezo ya sakata hilo alioomba apigiwe simu jioni.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU