CHAMA
Cha Wananchi (CUF) kimemuonya Waziri wa Nishati na Madini Professa
Sospeter Muhongo na kumtaka atambue kuwa katika suala hili la Gesi,
wananchi wa Mtwara ndiyo watashinda na Gesi lazima inufaishe taifa ikiwa
palepale Mtwara na hakuna haja ya kuendelea kuwaonea wananchi wa mikoa
ya pembezoni kwa kisingizio cha kulinda mshikamano wa kitaifa.
Akizungumzia sakata hilo la gesi ya Mtwara Naibu Katibu Mkuu Julius Mtatiro, alisema kuwa kunamshikamano gani wa kitaifa Mtwara ikiwa mikoa ya kusini inashughulikiwa na serikali ya CCM kila kukicha.
Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo.
"Wameshughulikiwa
kwenye korosho na kuacha mkulima wa korosho awe masikini huku Matajiri
wachache wanaoikusanya wakitajirika na kutoa 10% kwa viongozi wa CCM,
wamewashughulikia wakulima wa ufuta na hivi sasa hawana mbele wala
nyuma. Hata gesi nayo lazima ije DSM ?.
Ya songosongo inatosha kuja DSM, hii ya Mnazi Bay iachwe"alisema Mtatiro
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog