
CHADEMA wamesema kauli 
iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye kwamba 
Chadema kitakufa kutokana na kuwa na Sumu ya Ubaguzi haina ukweli 
wowote, na wamemtaka kiongozi huyo kutafakari zaidi kauli hiyo kwa 
maslahi ya Chama chake.
Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo 
wa CHADEMA BENSON KIGAILA anasema CHADEMA haiwezi kufa kwa dhana 
iliyozungumzwa na Nape na badala yake Chama hicho tawala ndicho 
kinachoweza kufa kutokana na changamoto ikiwemo ufisadi.
Akikaririwa Benson amesema “anachodai yeye kwamba kuna 
ubaguzi ndani ya CHADEMA, tunataka tumwambie kwamba chama cha siasa 
kinakufa pale kinapoacha msingi wake, dhamiri yake na majukumu yake ya 
kusimamia malengo na maslahi ya Umma”
Kwenye mistari mingine
 Chadema imemtaka Naibu Katibu wa CCM Mwigulu Nchemba kutoa ushahidi wa 
kauli aliyoitoa hivi karibuni kwamba Chadema  imekuwa ikipanga mipango 
ya mauaji.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog