Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony akisota kuokoa mpira
uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete kwa
njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele
mpaka dakika 90 kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye
mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa
CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji
wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio
uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa
mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na
hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji
wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio
uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry
Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu
ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya
Afrika Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba
jijini Mwanza.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry
Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry
alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
Nginja nginja tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kumalizika
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog