Facebook Comments Box

Friday, July 18, 2014

WAFADHILI KUREJESHA MSAADA UGANDA IKIWA.........

Wahisani wamesema wameridhika na kazi ya serikali mwaka 2012/13

Mapema mwaka huu wafadhili kadha walikata msaada wao wa bajeti kupinga sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja iliyopitishwa Februari. Wiki jana serikali ilitoa andiko linalojaribu kubainisha sheria hio dhidi ya wapenzi wa jinsia moja. 

Mnao siku ya Jumanne, wafadhili hao walionyesha kuridhika na kazi ya serikali mnamo mwaka wa fedha 2012/13, baada ya uhakiki wa kila mwaka kuhusu matendo ya serikali. Uhakiki huo unakusudiwa kuwapa fursa wafadhili kuamua ikiwa au la waendelee kugharimia bajeti ya Uganda kwa mamilioni ya dola.

Kwa jumla kasoro ya 20% ya bajeti ya Uganda inategemea misaada ya wafadhili. Wafadhili hususan kutoka Ulaya ambao husaidia bejeti ya Uganda walisitisha msaada wao kufuatia ripoti za ufujaji wa pesa za serikali pamoja na kupitishwa kwa sheria ya kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. Nchi hizo kiwawakilishwa na Denmark pamoja na beki ya dunia wanaonekana kushawishika kuendelea kusaidia Uganda baada ya kukutana na waziri mkuu Amama Mbabazi.
Nyingi ya pesa inazopata Uganda kama msaada hutumiwa katika miradi ya afya Katika taarifa yao ya pamoja, wahusika wote walitambua jukumu la Uganda katika kuweka amani na uthabiti katika kanda nzima na kuhimiza uhuru wa kujieleza pamoja na uwazi katika masala ya usimamizi wa pesa za msaada.

Wamejitolea kuendelea kufadhili Uganda kwa kima cha dola milioni arobaini katika siku zijazo. Marekani pamoja na nchi nyinginezo kutoka Ulaya zilisitisha msaada wa mamilioni ya dola baada ya Rais Museveni kutia saini sheria ya mapenzi ya jinsia moja mapema mwezi huu. Nchi hizo zinataka Uganda ifutilie mbali sheria hio kabla ya kuanza kuipa tena msaada. 

Wiki jana Waziri wa mambo ya nje wa Uganda alitoa taarifa kusema kuwa sheria hiyo ilitafsiriwa visivyo kwani lengo lake ni kuwalinda watoto bali sio kumbagua yeyote, wala haijulikani ikiwa tamko hilo ndilo lililoifanya wahisani kuanza tena kutoa msaada.


Wednesday, July 16, 2014

HABARI NJEMA KATIKA VITA DHIDI YA VVU

Virusi sugu vya HIV

Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.

 Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka. Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV. Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001. Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV.
CHANZO: BBC


KUPATA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA INGIA HAPA

Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 yaliyofanyika tarehe Mei 5 –
21, yametoka.
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa
waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana waliofaulu
ni 12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia 12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.


SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa


SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaliua
10. Osward Mang'ombe




Tuesday, July 15, 2014

ISRAEL YAANZA TENA KUISHAMBULIA GAZA

 Israel imeanza tena kushambulia Gaza ikidai kuwa Hamas inaishambulia licha ya mkataba wa kusitisha vita kufikiwa. Awali Israel ilikubali kusitisha vita kufuatia pendekezo la Misri kwa
pande zote mbili kusitisha vita Jumanne asubuhi. Hata hivyo, kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Gaza, lilikataa makubaliano hayo na kusema ni kama kusalimu amri.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu 192 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku nane zilizopita ili kukomesha wapiganaji wa Hamas kuusha makombora nchini Israel.

Raia wanne wa Israel wamejeruhiwa vibaya tangu mashambulizi hayo kuanza , lakini hakuna taarfa zozote za vifo.
Wizara ya usalama nchini Israel imesema kuwa roketi 50 zimerushwa ndani ya Israel tangu isitishe vita. Mashambulizi ya hivi punde yamepiga maeneo mawili katika ukanda
wa Gaza. Kundi la Hamas lilisema kuwa hawajapokea pendekezo lolote la kusitisha mashambulizi.

Aliongeza kwamba Hamas inahitaji masharti yake yote kukubaliwa kabla ya kukubali kusitisha vita.
Idara ya usalama nchini Israel imekubali mapendekezo hayo lakini ikasisitiza kuwa itaendelea kushambulia Gaza ikiwa Hamas watasitisha kusidhambulia kwa roketi.


IPTL WATAKA KAFULILA AWALIPE BILIONI 310

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imemfungulia kesi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikimtaka aombe radhi na kulipa fidia ya Sh bilioni 310. Katika kesi hiyo ya madai, Kafulila anadaiwa kuidhalilisha kampuni hiyo, kutokana na kauli alizotoa dhidi yake (IPTL).
IPTL na walalamikaji wengine Pan Africa Power Solution (PAP) na Mkurugenzi wa PAP, Harbinger Seth wanamlalamikia Kafulila kuwatuhumu kuchukua fedha kinyume cha sheria katika akaunti ya
Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Walalamikaji hao kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wamefungua kesi hiyo, wakitaka Kafulila awalipe Sh bilioni 210 kama fidia ya kutoa kauli za udhalilishaji,  kuwasababishia hasara katika biashara na kuharibu mtazamo wa biashara zao. Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila, awaombe radhi, pia awalipe Sh bilioni 100 kama hasara ya jumla pamoja na usumbufu
walioupata, kutokana na kauli za udhalilishaji. Kwa mujibu wa hati ya madai,  iliyopatikana mwishoni mwa wiki, Juni mwaka huu Kafulila alitangaza kuwa IPTL na Seth, walijipatia fedha kutoka akaunti ya Escrow kinyume cha sheria na kumuita Seth ni 'Singasinga', jambo lililomdhalilisha na kumharibia muonekano wake na biashara yake.

Walalamikaji hao wanadai kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,  bila kuwa na haki, Kafulila alitoa taarifa hizo, kuwa IPTL inajihusisha na biashara zisizo halali na za uongo, jambo
lililosababisha jamii kuamini na kuwaharibia mtazamo wa kibiashara. Aidha, wanadai  Kafulila akiwa mbunge alipoteza kinga ya wabunge inayowalinda wakizungumza bungeni, kwa kuwa alitoa taarifa hizo nje ya shughuli za Bunge.

Walidai Kafulila anaendelea kutoka taarifa hizo,  licha ya kumpa taarifa kwa maneno na maandishi, wakimtaka kuacha kufanya hivyo, kwa kuwa anawaharibia biashara kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa hati ya madai, IPTL iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye shirika hilo, lakini kulitokea mgogoro kati ya IPTL, Kampuni ya VIP Engineering and Marketing na Tanesco, jambo lililosababisha wafike Mahakama Kuu. Kutokana na mgogoro huo, Mahakama iliamuru Sh bilioni 200 zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow, zisitolewe hadi kesi hiyo itakapokwisha na baada ya kesi kuisha, Mahakama iliamuru IPTL ichukue fedha hizo.

Walalamikaji hao wanadai licha ya Kafulila, kujua kuwepo kwa mgogoro huo, aliendelea kutoa tuhuma hizo, huku akijua kuwa IPTL imechukua fedha hizo kwa amri halali ya Mahakama. Wakili huyo alisema wateja wake, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila awalipe Sh bilioni 310 kama fidia, aombe radhi, alipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo na amri nyingine, ambazo
Mahakama itaona zinafaa.


PICHA NA VIDEO YA DUKA LINALO UNGUA MWANANYAMALA MUDA HUU





MUQAWAMA WATUMA NDEGE ISIYO NA RUBANI TEL AVIV

Brigedi ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa, wahandisi wake wamefanikiwa kutengeneza ndege isiyo ya rubani kwa jina la Ababil 1. Ripoti iliyotolewa na brigedia hiyo hii leo, imeeleza kuwa, ndege hiyo imefanikiwa kuruka juu ya jengo la idara ya Wizara ya Vita ya utawala haramu wa Kizayuni mjini Tel Aviv. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ndege hiyo isiyo na rubani ni moja kati ya ndege tatu zenye kazi tofauti zilizoundwa na wapiganaji wa muqawama wa Kipalestina. Aidha imezitaja ndege hizo kuwa ni pamoja na ndege ya kijasusi inayofanya kazi za kuchukua habari mbalimbali za adui, ndege ya kutekeleza hujuma na mashambulizi na ya tatu ni ndege inayosheheni mada za miripuko na kujiripua katika eneo maalumu la adui. Imeelezwa kuwa ndege hiyo iliruka mapema leo asubuhi katika shughuli zake za kiupelelezi ambapo iliweza kutuma ripoti muhimu, suala ambalo limeutia kiwewe utawala huo bandia. Kwengineko Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, watu 173 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huku wengine 1, 200 wakijeruhiwa. 

Idadi hiyo imeongezeka kufuatia watu saba kuuawa shahidi hii leo akiwemo mtoto mchanga huku kijana mwingine akiuawa katika shambulizi la anga katika eneo la Rafah.

Wakati huo huo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ameutaka Umoja wa Mataifa kuwasaidia Wapalestina. Abbasi ametoa ombi hilo kupitia barua aliyoiwasilisha kwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Robert Serry akimtaka awasilishe ujumbe huo kwa Katibu Mkuu wa umoja huo. Abbasi amesema kuwa, serikali ya Palestina imekwishachukua maamuzi maalumu ambayo yatatangazwa hivi karibuni kuhusiana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.


Sunday, July 13, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA KUSINI AJIUZURU

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kanda ya  kusini  ambaye pia ni Mchungaji  wa Kanisa la Avangelisitic Assemblies of God Tanzania(EAGT),Joseph Matare amejiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na Kanisa lake hilo Kuagiza
Wachungaji wake ambao ni Viongozi wa  Vyama vya Siasa kuachana na Nafasi zao za Kisiasa. Joseph Matare akizungumza na Waandishi wa habari Mjini Songea amesema kuwa ameamua kujuzulu Nafasi yake ya Uongozi wa CHADEMA Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kufuatia  Kanisa lake katika Mkutano wake wa Kanda kuagiza Wachungaji wake wote ambao ni Viongozi wa Kisiasa kuachia nafasi zao na badala yake wasimamie Kazi ya Mungu Katika Makanisa yao. ‘Kufuatia maagizo ya Mkutano huo wa Kanisa uliofanyika Njombe nimeamua kutii na  leo tarehe 10 Julai  2014 nimeamua kujiuzulu na Katibu wangu Mkuu Dr Wilbroad Slaa nilimjulisha tangu tarehe 04 Juni mwaka huu’ alisema  Matare katika taarifa yake ya kujiuzulu. 

Anafafanua kuwa muda  wa Viongozi wa Kanda ulikuwa ni wa muda na wa mpito hadi  uchaguzi wa Kanda utakapopita ambao ulipaswa kufanyika Juni 2014 na kwamba muda umeongezwa hivyo ameona aheshimu  maagizo yaliyomuweka madarakani. Hata hivyo Matare anasema kuwa anawatia moyo Makamanda wote wa CHADEMA  waliobaki kuendelea kupigania Nchi ili iondokane na uovu  unaotendeka sasa na kwamba Mungu atakuwa nao wale wote wanaotafuta haki kwa ajili ya Wananchi walio wengi.

Anasema  kuwa ameondoka bila kuwa na Ugomvi na Kiongozi yeyote wa CHADEMA   hivyo wataendelea kushirikiana kutafuta  haki akiwa Mwanachama wa Kawaida na Mchungaji. 

Matare ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT  Mkuzo la Mjini Songea la Mkoani Ruvuma  amesema kuwa anatambua juhudi za Viongozi wa CHADEMA katika kupigania haki za Wananchi na
Wabunge wote wa CHADEMA katika kupigania haki na kwamba ipo siku Mungu atawalipa ujira wa kazi wanayofanya. Anasema kuwa Mungu anatambua kazi  nzito wanayofanya Viongozi wa CHADEMA ambayo amesema ni ya kutafuta Ukombozi kamili wa Nchi na itakuwa  ni uendawazimu kubeza kazi hiyo.


Saturday, July 12, 2014

AJALI ENEO LA UBUNGO MATAA MUDA HUU

Gari la mchanga lililokuwa likitokea maeneo ya kimara limemshinda dereva wakati wa kukata kona kutoka barabara ya Morogoro kuingia barabara ya Mandela hapa eneo la Ubungo. Hakuna mtu aliye fariki bali ni majeraha machache kwa dereva.




Friday, July 11, 2014

DIAMOND PLATNUMZ APOKELEWA KWA SHANGWE NA BASHASHA AKITOKEA MAREKANI

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania maarufu kama Bongo Fleva Naseeb Abdulmalik a.k.a Diamond Platnumz aliwasili jana tarehe 10/07/2014 akitokea Marekani alikokwenda kwa ajili ya kushiriki katika tuzo za BET ambazo hufanyika kila mwaka.

Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria na yeye kuishia kupata cheti cha ushiriki ambapo kwake sio vibaya maana anaamini huo ni mwanzo mzuri kwake wa kuelekea katika mafanikio.


Baada ya kuwasili Diamond aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa safari yake ilikuwa nzuri na amejifunza mambo mengi sana pia amekutana na watu wengi na tutarajie mengi mazuri katika muziki wetu.

Na kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, ambayo inafanya vema kwenye vituo vya luninga hapa nchini kwa sasa.


Tuesday, July 8, 2014

BOMU LALIPUKA ARUSHA NA KUUWA NA KUJERUHI

Taarifa zilizotufikia za kusikitisha zinasema kwamba kumetokea mauwaji katika mgahawa wa Wama ulioko Gymkhana jijini Arusha (Pichani chini). Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha watu zaidi ya 8 kujeruhiwa vibaya, idadi ya waliopoteza maisha bado haijajulikana, majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya Seliani jijini Arusha.




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU