Facebook Comments Box

Tuesday, July 15, 2014

MUQAWAMA WATUMA NDEGE ISIYO NA RUBANI TEL AVIV

Brigedi ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa, wahandisi wake wamefanikiwa kutengeneza ndege isiyo ya rubani kwa jina la Ababil 1. Ripoti iliyotolewa na brigedia hiyo hii leo, imeeleza kuwa, ndege hiyo imefanikiwa kuruka juu ya jengo la idara ya Wizara ya Vita ya utawala haramu wa Kizayuni mjini Tel Aviv. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ndege hiyo isiyo na rubani ni moja kati ya ndege tatu zenye kazi tofauti zilizoundwa na wapiganaji wa muqawama wa Kipalestina. Aidha imezitaja ndege hizo kuwa ni pamoja na ndege ya kijasusi inayofanya kazi za kuchukua habari mbalimbali za adui, ndege ya kutekeleza hujuma na mashambulizi na ya tatu ni ndege inayosheheni mada za miripuko na kujiripua katika eneo maalumu la adui. Imeelezwa kuwa ndege hiyo iliruka mapema leo asubuhi katika shughuli zake za kiupelelezi ambapo iliweza kutuma ripoti muhimu, suala ambalo limeutia kiwewe utawala huo bandia. Kwengineko Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, watu 173 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huku wengine 1, 200 wakijeruhiwa. 

Idadi hiyo imeongezeka kufuatia watu saba kuuawa shahidi hii leo akiwemo mtoto mchanga huku kijana mwingine akiuawa katika shambulizi la anga katika eneo la Rafah.

Wakati huo huo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ameutaka Umoja wa Mataifa kuwasaidia Wapalestina. Abbasi ametoa ombi hilo kupitia barua aliyoiwasilisha kwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Robert Serry akimtaka awasilishe ujumbe huo kwa Katibu Mkuu wa umoja huo. Abbasi amesema kuwa, serikali ya Palestina imekwishachukua maamuzi maalumu ambayo yatatangazwa hivi karibuni kuhusiana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU