Mapema mwaka huu wafadhili kadha
walikata msaada wao wa bajeti kupinga sheria kali dhidi ya wapenzi wa
jinsia moja iliyopitishwa Februari. Wiki jana serikali ilitoa andiko linalojaribu kubainisha sheria hio dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Mnao
siku ya Jumanne, wafadhili hao walionyesha kuridhika na kazi ya
serikali mnamo mwaka wa fedha 2012/13, baada ya uhakiki wa kila mwaka
kuhusu matendo ya serikali. Uhakiki huo unakusudiwa kuwapa fursa wafadhili kuamua ikiwa au la waendelee kugharimia bajeti ya Uganda kwa mamilioni ya dola.
Kwa jumla kasoro ya 20% ya bajeti ya Uganda inategemea misaada ya wafadhili. Wafadhili hususan kutoka Ulaya ambao husaidia
bejeti ya Uganda walisitisha msaada wao kufuatia ripoti za ufujaji wa
pesa za serikali pamoja na kupitishwa kwa sheria ya kuharamisha mapenzi
ya jinsia moja. Nchi hizo kiwawakilishwa na Denmark pamoja na
beki ya dunia wanaonekana kushawishika kuendelea kusaidia Uganda baada
ya kukutana na waziri mkuu Amama Mbabazi.
Wamejitolea kuendelea kufadhili Uganda kwa kima cha dola milioni arobaini katika siku zijazo. Marekani pamoja na nchi nyinginezo kutoka Ulaya
zilisitisha msaada wa mamilioni ya dola baada ya Rais Museveni kutia
saini sheria ya mapenzi ya jinsia moja mapema mwezi huu. Nchi hizo zinataka Uganda ifutilie mbali sheria hio kabla ya kuanza kuipa tena msaada.
Wiki jana Waziri wa mambo ya nje wa Uganda
alitoa taarifa kusema kuwa sheria hiyo ilitafsiriwa visivyo kwani lengo
lake ni kuwalinda watoto bali sio kumbagua yeyote, wala haijulikani
ikiwa tamko hilo ndilo lililoifanya wahisani kuanza tena kutoa msaada.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog