Facebook Comments Box

Saturday, July 13, 2013

KIIZA ATUA LEO JIONI KUSAINI YANGA MIAKA MIWILI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego wa Kampala’ anatua Alasiri ya leo Dar es Salaam na ndege ya KQ tayari kusaini Mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga SC kwa miaka mingine miwili.  Hiyo inafuatia mpachika mabao huyo kufikia makubaliano na Yanga juu ya dau la usajili, baada ya awali kushindana hadi akarejea kwao, Kampala na ikaripotiwa alikuwa karibuni kusaini URA ya kwao. Mfanyabiashara mwenye jina mjini, Mussa Katabaro alikwea pipa hadi Uganda wiki mbili zilizopita kufanya mazungumzo ya kina na Kiiza ili abaki Yanga na hatimaye akakubali kuendelea kuvaa jezi za kijani na njano kwa miaka mingine miwili.
Anarudi; Hamisi Kiiza anatua leo
Katabaro ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC na mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba Kiiza anatua na ndege ya shirika la Kenya, KQ Alasiri. Katabaro alipokuwa Kampala katika mazungumzo yake na Diego walikubaliana kumuongezea Mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 na mshahara wa dola 1,500 kwa mwezi. Lakini Katabaro akaomba Kiiza akubali kuchukua dola 20,000 kwa sasa na dola 20,000 nyingine atampa katika mwanzo wa mwaka wa pili wa Mkataba wake. Kiiza akasema anataka dola 40,000 kamili kwa sababu ana kitu anataka kufanya na ndiyo maana alikataa kupokea dola 35,000 na gari, ilia pate fedha kamili. URA  ilikuwa tayari kumsaini Kiiza kwa mshahara wa dola 1,000 na dau la usajili dola 40,000 kama ambazo ameahidiwa Jangwani. Awali, Kiiza aligoma kusaini Yanga kutokana na kulazimishwa achukue dola 35,000 na dola 5,000 nyingine apewe gari.



HIVI NDIVYO CHADEMA WATAKAVYO TOA MSIMAMO WAO KUHUSU KATIBA MPYA LEO

Msimamo wetu kuhusu rasimu ya katiba mpya na mustakabali wa taifa utatolewa leo Jumamosi ya Julai 13, 2013 kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Ukombozi-Manzese kuanzia saa 8 mchana.

Hotuba zitatolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Dk.W.Slaa, T.Lissu, M.Marando nk nathibitisha nami nitakuwapo kuwakaribisha Jimboni Ubungo.

Wananchi wote mnakaribishwa. Njoo wewe, njoo na yule!

Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli!

Muhimu: 
  • Shule ipo jirani na Manzese TipTop. 
  • Maelekezo wasiliana na M/Kiti wa Kata ya Manzese, Ali Makwilo 0784-691449 au 0715-691449 au 0769-658593

---
Taarifa hii imetolewa na:
John Mnyika (Mb)
Jumamosi, Julai 13, 2013



KIJANA WISEMAN LUVANDA ATEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR ES SALAAM

Wiseman Luvanda (23) akiwasili jijini Dar es Salaam alitokea Mbeya kwa miguu.Akiwa anaiunga mkono Timu ya Taifa


Watu wakimpokea kwa shangwe kijana aliye onesha uzalendo wa hali ya juu

Kijana Wiseman Luvanda(23) akikamilisha safari yake ya kutoka Mbeya hadi Dar kwa miguu! Kauli mbiu yake ni "Tanzania nchi yangu,Taifa Stars Timu yangu, Amka wakati wa Uzalendo ni Sasa". Tumefanya nn kuienzi nchi?

SIMBA YAMSAJILI HAMISI TAMBWE

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi.

Tambwe ambaye pia alikuwa akiwania na mabingwa wa Tanzania bara Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.
Tambwe amesaini mkataba huo mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba.


Friday, July 12, 2013

OPRAH WINFREY KUJA TANZANIA KESHO

. 
Inaelekea President Obama kaacha upepo mzuri Tanzania manake taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita baada tu ya bondia Evander kuthibitishwa na yeye kuja Tanzania, mtangazaji staa wa dunia Oprah Winfrey nae anatarajiwa kufika Tanzania.
Staa huyu ambae amewahi kufanya interview na mastaa wengine kama marapper  Jay Z na 50 Cent, unaambiwa usitegemee kumuona Dar es salaam au sehemu nyingine maarufu za town, anatua Serengeti kesho July 13 2013 kwa ajili ya mapumziko tu na kuondokea hukohuko.


TANGAZO LA AJIRA KUTOKA UTUMISHI


Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Tanzania Dairy Board, Tanzania Institute of Accountancy, College of Business Education, National Institute of Transport, Tanzania Broadcasting Cooporation, Tanzania Institute of Education, Tanzania Library Services Board, Local Government training Institute, Institute of Finance Management, National College of Tourism Agency, Law school of Tanzania, Tanzania Metrological Agency, Moshi Unoversity college of cooperative and business Studies, Dar es Salaam Marine Institute, Kibaha Education Centre, Institute of Rural Develepment Planning, Tanzania Public Service College, Tanzania Wildlife Research institute, Institute of Accountancy Arusha na National Examination Concil of Tanzania inawatangazia furasa mbalimbali za Ajira Serikalini, Kwa maelezo zaidi fungua kwenye TOVUTI ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo ni www.ajira.go.tz. 


TANGAZO LA KAZI-JULY 2013

PICHA: WABUNGE WAKIPIGANA BUNGENI


Hawa ni wabunge wa Ukraine wakipeana makonde bungeni

POLISI WAFANYA UPELELEZI KUMPATA ALIE RUHUSU KILO 150 ZA MADAWA YA KULEVYA KUPITA AIR PORT

Akizungumza na gazeti la NIPASHE lililochapisha habari ya dawa za kulevya kilo 150 zilizokamatwa kwa wasichana wa Kitanzania nchini Afrika Kusini, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit Kato, amesema tukio hilo ni baya, limeifedhehesha Tanzania na kuiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu.

Hivyo amesema kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.

“Ni lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni  mapema mno kuinyoshea kidole taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa na gazeti hili kama wasichana hao walikaguliwa.

Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.

Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.

Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).

“Tukio hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na kuongeza: "Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini."

Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na   Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.



Thursday, July 11, 2013

VIDEO: MWANAMKE AKIMPIGA MUME WAKE HADHARANI

.
.
Ni ngumu kumuona mwanaume akitokwa machozi kama hivi…. hii imetokana na mke wake kumpiga makofi hadharani kwenye mji wa Meru nchini Kenya ambapo Mwanamke huyo alikua anadai jamaa kamkana, japo anasisitiza kwamba ni mume wake na ndio baba wa watoto mapacha akiwemo mmoja alienae mgongoni, Mwanaume alikataa kabisa na kusema hata watoto sio wake.
Taarifa ambayo imerushwa na KTN Kenya, ni kwamba alichotaka Mwanamke ni Mwanaume huyo akubali tu kwamba ni mume wake na pia ndio baba watoto wa mapacha hao… lakini Mwanaume aliapa kabisa kwamba hausiki kwenye upande wowote, hicho ndio kilichompa hasira Mwanamke na kuanza kumpiga na baadae pia kusaidiwa kupiga na Mwanamke aliekua nae.
Kenya imekua kwenye mfululizo wa kesi za Wanawake kupiga waume zao nyumbani na hadharani pale wanapokosana ambapo February 2012 Umoja wa Wanaume Kenya ulitangaza kususia kula majumbani kwa wiki moja na kununua chakula hotelini mpaka Serikali itakapoingilia usawa wa Wanaume na kuhakikisha tabia ya Wanawake kupiga Waume zao inamalizwa.





MAWAIDHA: NAMNA YA KUSWALI NA SHEIKH RAMADHAAN KURIA BIN KAGUO




AKODI NDEGE YA KIFAHARI KWA MILIONI 162 KUMSAFIRISHA PAKA WAKE

Paka mwenye jina Marsik wa Urusi amesafirishwa na ndege binafsi ya Paramount Business Jets (PBJ), kutoka Urusi hadi Marekani kwa gharama ya dola laki moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 162 za Tanzania.
Akisafiri kutoka Urusi hadi Marekani, Marsik anadaiwa kupata huduma ya nguvu kabla hajapanda na ndani ya ndege hiyo.
Vyeti vyake vya afya vinavyoonesha chanjo alizopata alivipata saa 24 kabla ya safari kuanza.
Tajiri huyo anadai kutumia kiasi chote hicho ili kuhakikisha kuwa paka wake anafika Marekani salama na kuepuka kunyanyasika ama kifo kwakuwa baadhi ya wanyama wanaosafiri kwa ndege za kawaida huwekwa kwenye sehemu ya mizigo hupoteza maisha.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU