Facebook Comments Box

Friday, July 12, 2013

POLISI WAFANYA UPELELEZI KUMPATA ALIE RUHUSU KILO 150 ZA MADAWA YA KULEVYA KUPITA AIR PORT

Akizungumza na gazeti la NIPASHE lililochapisha habari ya dawa za kulevya kilo 150 zilizokamatwa kwa wasichana wa Kitanzania nchini Afrika Kusini, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit Kato, amesema tukio hilo ni baya, limeifedhehesha Tanzania na kuiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu.

Hivyo amesema kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.

“Ni lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni  mapema mno kuinyoshea kidole taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa na gazeti hili kama wasichana hao walikaguliwa.

Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.

Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.

Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).

“Tukio hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na kuongeza: "Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini."

Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na   Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU