Facebook Comments Box

Saturday, March 7, 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI NA KUANZA KAZI YAKE MAPEMAA

Kevin McGill

Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Kevin McGill Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.

Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa 

wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewashtua watu wengi na kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wamepigwa na butwaa kwa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. 

Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU