Facebook Comments Box

Thursday, August 21, 2014

HUMAN RIGHT NA HIZB-UT-TAHRIR WAILALAMIKIA KENYA KWA KUUWA WAISLAM

Kwa mara nyengine kikosi cha kupambana na ugaidi kimekashifiwa na kulaumiwa vikali kwa kuhusika na matendo ya kikatili dhidi ya Waislamu. Likizindua taarifa yake siku ya Jumatatu tarehe 18/08/2014, shirika la utetezi la haki za binadamu limeshtumu kitengo hicho kwa kutekeleza mauaji,utekaji nyara pamoja na kuwapoteza washukiwa wa ugaidi. 
“Kikosi cha kupambana na ugaidi kinawauwa watu waso na hatia na kuwapoteza wengine tena mbele ya maafisa wakuu wa serikali, ofisi kubwa za kiubalozi na zile za umoja wa mataifa…” Akasema Bi Leslie Lefkow naibu mkurugenzi wa shirika hilo.

Kufuatia taarifa hii Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inaeleza yafuatayo:-

- Taarifa hizi sio ngeni kwani jamii ya Kiislamu na ya Kenya kwa ujumla. ATPU tokea ibuniwe mwaka 2003, imekuwa ikiyafanya maovu haya paruwanja pasina na kushikwa na hisia ya ubinadamu! Mfano wa uovu walioufanya mchana peupe ni kule kumtia mbaroni kijana Suleiman Swaleh Salim wa Majengo Mombasa akitoka swala ya ijumaa mapema mwezi huu. Hadi wa
leo familia yake haijui yuko wapi? Wanawake wamekuwa wajane,watoto kuwa mayatima na nyumba kubakia pasina barobaro! Na kila ATPU inapo ambiwa iogope Mungu na ikome kufanya mauaji haya hupandwa na mori wa kufanya zaidi
madhambi hayo.

- Mauaji haya ni moja wapo tu ya dhulma kubwa inayotendewa jamii ya Kiislamu ya Kenya. Na imekuwa si tu maafisa wa ATPU bali unyama huu umetapakaa hadi kwa vikosi vyengine vya polisi.
Kwa mfano katika mtaa wa Eastleigh Jijini Nairobi, polisi wa kikosi cha GSU walikuwa wakivamia majumba na kuwapiga Waislamu
wenye asli ya Kisomali na kwenda kuwalaza kwenye baridi kali uwanjani Kasarani. Dhulma hizi zilifanywa kwa kile kilichoitwa oparesheni ‘Usalama Watch’ mwezi Aprili mwaka huu.

- ATPU imetekeleza unyama huu ndani ya dhamana ya Marekani,taifa lenye historia mbovu ya mauaji ya Waislamu ,mfadhili mkubwa wa  vita hivi kote ulimwenguni. Mbali na Marekani kutoa mafunzo kwa vikosi mbali mbali  kwa madai ya kupambana na ugaidi, aidha hufadhili kifedha mataifa na taasisi zake za kiusalama ati kupambana ‘ugaidi’. Kwenye taarifa ilioandaliwa kwa ushirikiano wa mashirika mawili ya kutetea haki za binadamu,; Open Society Justice Initiative na Muslim For Human Rights (Muhuri) yalidokeza kuwa katika mwaka ulioanzishwa kikosi hiki cha ATPU kilipewa kitita cha $ 10 milioni kutoka Marekani. Na bila shaka hadi sasa kikosi hiki kinaendelea kupata ufadhili kutoka Marekani.

Mwisho tunawakumbusha Waislamu kuwa mateso haya dhidi ya Waislamu wa Kenya ni sehemu tu mateso yanaowakubwa Waislamu wote duniani. Kwa hakika lau tutaandika taarifa za mauaji ya Waislamu kwenye vita hivi basi tutachukua muda na kujaza vitabu vingi. Ni muhimu kuelewa kuwa vita hivi ni kampeni
ya kuzuia Uislamu usisimame kuongoza dunia huku Marekani aendelee na kukoloni dunia kimawazo na kivitendo. Cha msingi ni kuelewa kuwa Waislamu ndio walengwa katika vita hivi kwa kuwa wana mfumo safi ulio na uwezo kuongoza Ulimwengu na kung’oa mfumo wa kikoloni wa kibepari unaongozwa na Marekani. Hivyo ni muhimu kupaza sauti yetu kwa pamoja kila tunapokumbwa na madhila haya huku tukifanya kazi ya kuregesha mfumo wetu kuongoza maisha jumla ya wanadamu chini ya kiongozi Khalifa atakayezuia dhulma za wenye kudhulumu na kueneza haki kwa walimwengu wote.

KUMB: 20/1435AH    24 Shawwal, 1435 Hijri  20-08-2014

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir East Africa

Tel:  +254 720  597 841 +254 0789 574 608

E-mail: media@hizb-eastafrica.com
Official website of Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Media office website of Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.info


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU