Wiki moja kabla ya kupewa dhamana Mh. Mansour Yusuph Himid katika mkutano wa Chama cha wananchi Cuf uliofanyika kwenye viwanja vya Demkokrasia Kibanda maiti mjini Unguja alitangazwa kuwa ni shujaa tena kidume haswaa, hayo yalisemwa na Mh.Ismail Jussa Ladhu pale aliposimama na kuzungumzia kwa ufupi juu ya kukamatwa kwa waziri huyo wa zamani wa serikali ya Smz, mh.Jussa alisema kuwa walipokuwa wamempelekea chai ya asubuhi bw. Mansour aliwaambia wasimletee tena chai kwa kuwa atakunywa tu uji wa kule gerezani na kuwa uji ule wa gerezani ni mtamu sana huku akimalizia kwa kumwita ni shujaa tena kidume hasa.
Maalim Seif yeye kwa upande wake akimzungumzia mh. Alisema kuwa Mansour Yusuph Himid wote tunajua kuwa ni raia wa Zanzibar kazaliwa Zanzibar na baba yake ni miongoni mwa wanamapinduzi, waliokuwa hawamjui wajue hivyo, ametoka katika mifupa ya wanamapinduzi, kapatwa na mtihani kakamatwa na sasa hivi yuko jela, Na mh. Jussa amewaambia kuwa kwenda jela ni ishara nzuri, niwaulizeni nabii Yusuph hakwenda jela? Sasa ikiwa mitume walikwenda jela itakuwaje sisi? Yanayo mkuta Mansour leo hii wanampitisha kwenye njia zile zile walizompitisha Maalim seif, Maalim Seif kwanza alifukuzwa Chama, kama vile haitoshi wakamtafutia shitaka halina dhamana wakamuweka jela kwa muda waliotaka wenyewe ulipofika muda wakaniambia toka, lakini wakaniambia unatoka lakini huna ruhusa ya kuzungumza kwenye mikutano ya hadhara nikaitikia Inshaallah, tumeanzisha Cuf mkutano wa kwanza tumeufanya malindi pale mimi nipo kama makamu mwenyekiti lakini ndiyo nilifungwa mdomo nilikuja kwenye jukwaa pale nyote mnakumbuka nikatoa mkono tu wakaenda wenyewe mpaka wakaamua basi sasa kesi tunaifuta na maalim Seif Yule Yule sasa ni makamu wa rais wa Zanzibar.
Nakumbuka wakati ule napelekwa jela askari walikuwa wananitukana na kuninyanyasa mie kimyaa kabisa lakini mungu si Athumani wala si Msaki mmoja wao yupo Dar es salam pale akiniona sasa hivi anapiga saluti, kwa hivyo nasema na Mansour ni ishara njema na hatujui mwenyezimungu huko mbele kamuandikia nini ,lakini najua kamuandikia mambo mema Inshaallah, lakini papo hapo niseme nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu yeye si mwanachama tena wa chama cha mapinduzi, nataka niamini kwamba Mansour kakamatwa kwa sababu ametoka hadharani na kuunga mkono mamlaka kamili kwa Zanzibar, nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema wazi wazi kwamba atamuunga mkono maalim Seif mwakani kwenye uchaguzi, nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema atagombea jimbo la Kiembe samaki kwa tiketi Cuf, Nataka niamini kuwa hizo siyo sababu hizo siyo sababu zilizofanywa Mansour akamatwe, Nataka niamini kwamba Mansour atatendewa haki kama raia yoyote mwingine katika nchi hii na kwamba yale mashitaka yote yanayomkabili basi sheria itachukua mkondo wake pasiwepo na shinikizo za kisiasa,akitoa mfano kwenye kesi Maalim seif alisema yeye siku moja ya kesi hakimu anayehusika alikuwa anakutana watu kwenye ofisi ya waziri kiongozi halafu wanaamua kesho tukafanye kwa maalim Seif, sasa nataka niamini hayo hayatatendeka kwa Mansour kwamba mahakama iliyo huru itaweza kabisa kusikiliza shitaka lilipo mbele yake kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, kwa sababu sasa hivi siyo tena mwaka 64, wala sasa hivi siyo tena mwaka 74 wala siyo tena 84 sasa hivi viongozi wote tunapiga kelele tunataka utawala wa sheria.
Tumeambiwa kabla ya kufa huajaumbika huyu mh. Mansour si alikuwa Waziri huyu na walikuwa wakimpigia saluti huyu si mwenzao? Sasa kama watu wapo walikula njama basi wajue mwenyezimungu anahukumu hapa hapa duniani Akhera inakwenda hesabu tu, kwa hivyo yaliyomfika Mansour yanaweza kumfika mtu yeyote sasa kama kuna watu kweli wamekula njama Mnsour akae ndani basi wajue kuwa wakati mwingine ukilitandika godoro uliloweka miba ili mwenzako aje alale basi ipo siku utakuja kulilalia wewe alimalizia maalim Seif.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog