Facebook Comments Box

Thursday, August 21, 2014

TANZANIA YAZINDUA MGODI WAKE WA KWANZA.

Waziri wa Nishati na Madini Mh Sospeter Muhongo
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake wa kwanza wa madini utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa watanzania.Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo.

Kwa kipindi sasa watanzania wengi wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira katika nafasi muhimu katika migodi ya hapa nchini. Watanzania wengine wakilalamikia migodi hiyo kutofaidisha nchi na kutowathamini wananchi wanao zunguka maeneo hayo na wengine wakilalamikia uharibifu wa mazingira wa migodi inayomilikiwa na wawekezaji.

Huwenda hii ikawa njia nzuri ya kuinua uchumi wa nchi pamoja na kukuza ajira kwa vijana wengi wa kitanzania walio maliza vyuo vikuu na kukosa ajira.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU