Facebook Comments Box

Friday, September 12, 2014

BREAKING NEWS: MSIKITI WA MTAMBANI UNAUNGUA TENA

Taarifa zilizo tufikia ni kuwa msikiti wa mtambani umepata mtihani tena baada ya kuungua moto. Chanzo cha moto huo hakijajulikana. Hamna majeruhi alie ripotiwa. Watu walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya swala ya Ijumaa ndio likatokea tatizo hilo
waumini wa kiislam wakifanya juhudi kuudhibiti moto huo.
Baada ya muda wa mwezi mmoja wa tukio la kuungua moto kwa majengo ya shule ya Mivumoni iliyoko katika msikiti wa Mtambani,
Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo kwa mara nyingine moto umezuka katika Ghorofa ya pili
ya jengo hilo.


Moto huo unaelezwa na mashuhuda kuwa ulianza muda wa saa sita na nusu za mchana
kabla ya kusaliwa swala ya ijumaa. Jitihada za
kuzima moto huo zilifanyika na kuzaa matunda.
Hata hivyo moto huo ulioanzia katika darasa lilokuwa linatumiwa na wanafunzi kama chumba
chumba cha dharura tangu tukio la awali,
Gari la Zimamoto lilifika wakati moto ushazimwa

gari la Zimamoto
 
Baada ya kuzimwa kwa moto huo taratibu za swala ya ijumaa ziliendelea kama kawaida.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila kumetokea sintofahamu kwa waumini wa msikiti
 huo ni nini hasa kilicho sababisha kuzuka tena
kwa moto huo hali ya kuwa jengo hilo limekosa
lhuduma ya umeme tangu kuzuke moto wa awali.

Jengo lililoshika moto leo
Kwa mara ya kwanza moto ulizuka siku ya jumatano jioni ya tarehe 13 Agosti 2014.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU