Facebook Comments Box

Friday, September 12, 2014

PATA KUFAHAMU HALI YA MCHEZAJI WA IVORY COAST BAADA YA VIPIMO

Serge Aurier akiwa chini baada ya kuanguka na kuzimia katika mpambano kati ya Cameroun na Ivory Coast

Mlinzi matata wa Ivory Coast amesema kuwa sawa na madaktari baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.Madaktari walitoa uamuzi wao baada ya Serge Aurier kujeruhiwa na kuzimia kwa muda wakati wa michuano ya kufuzu kwa kombe la taifa bingwa Afrika dhidi ya Cameroon Jumatano. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alijeruhiwa baada ya kugongana na kinara wa Cameroon, Stephane Mbia mapema wakati wa kipindi cha pili cha mechi kati ya timu zao.

Ivory Coast ilishindwa na Cameroon kwa mabao 4-1. Aliondolewa uwanjani kwa kitanda na alionekana kujeruhiwa vibaya. Lakini Aurier alipata fahamu na kubaki uwanjani kutizama mechi ilipokuwa ikiendelea.

"Alipokea matibabu akiwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, na msaada huo ndio ulimsaidia kupata fahamu kabla ya kurejea sehemu walipokuwa wachezaji wa akiba. ''


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU