Facebook Comments Box

Monday, September 23, 2013

ASKARI WATATU WAFARIKI BAADA YA GARI LA OPERESHENI KIMBUNGA KUPINDUKA

 
Picture
Miili ya Askari waliofariki ikiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama-Shinyanga.
Askari Polisi watatu wa Operesheni Kimbunga wamefariki dunia jioni ya tarehe 22/09/2013 siku ya Jumapili mjini Kahama baada ya kupata ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe. 

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi na hivyo kumshinda na kupinduka.

Majeruhi wanane wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama wakiwemo askari polisi sita na Maafisa Uhamiaji wawili, huku magari yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na kulala Kahama.
CHANZO:Wavuti


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU