Manchester United imefungwa mabao 4-1 na wapinzani wa Jiji,
Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad hapo jana.
Kocha David Moyes amekaribishwa vizuri na Manuel Pellegrini kwa mabao ya Sergio Aguero dakika ya 16 na 47, Yaya Toure dakika ya 45 na Samir Nasri dakika ya 50.
Wayne Rooney alitengeneza heshima kwa bao lake la kufutia machozi aliloifungia United dakika ya 78.
Kikosi
cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic,
Kolarov, Jesus Navas /Milner dk71, Toure, Fernandinho, Nasri,
Aguero/Javi Garcia dk86 na Negredo/Dzeko DK75.
Manchester United: De Gea 5, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Fellaini, Valencia, Rooney, Young/Cleverley DK51 na Welbeck.
Robin van Persie aliikosa mechi hiyo baada ya kuwa majeruhi kama unavyo muona jukwaani akitazama mechi hiyo.
Wayne Rooney, Danny Welbeck na Michael Carrickwakiwa wameshika viuno hawaamini baada ya kupigwa moja ya mabao katika mechi hiyo ya jana.
Rooney alifunga katika dakika kumi za mwisho na kuipatia Man U angalau bao la kufutia machozi na kufanya mpambano kuisha kwa 4-1.
Joe Hart akisalimiana na Rooney mwisho wa mchezo huo.
Rooney, Chris Smalling na David de Gea wakitoka uwanjani baada ya mechi kumalizika.
Moyes akiwa katika wakati mgumu katika mechi yake kubwa ya kwanza kabisa ya Jiji la Manchester ijulikanayo kama "Manchester derby".
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog