Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania kwa kufunga bao hilo pekee la ushindi jana.
Tanzania
ilikua kundi moja na Sierra-Leone, Malawi, na Uganda. Walishinda mechi
moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1, wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na
kutoka sare na Malawi 1-1.
Malkia wadogo; Tanzania wakiwa na Kombe lao baada ya ushindi |
Katika
Robo Fainali, mabinti wa kibongo wakashinda 4-2 kwa mikwaju ya penalti
dhidi ya DRC Uwanja wa NIS Sports, kabla ya kuifumua Uganda kwa mabai
8-1 kwenye Nusu Fainali.Mbali
na ushindi huo wa wasichana wa Tanzania walijishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji
bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora
kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.
Kwa
upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa baada ya
kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6 katika mechi ya fainali ya
Airtel Rising Stars ilifanyika kwenye uwanja wa Agege nchini Nigeria.
Mabingwa; Kikosi cha Tanzania wanawake |
Niger
wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi baada ya kushinda michezo
yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu
katika mechi sita. Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.
Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main Bowl.
Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu na yamekua bora kwa vijana wadogo na kwa kuzingatia jinsia.
CHANZO:BIN ZUBEIRI
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog