Facebook Comments Box

Monday, September 23, 2013

AZAM FC WAINYAMAZISHA YANGA SC YA JANGWANI KAMA HAWAPO VILE

 Kikosi cha Azam Fc kilichoifunga Yanga SC hapo jana Uwanja wa Taifa
Kikosi cha Yanga SC kilichofungwa hapo jana na Azam Uwanja wa Taifa

Baada ya Tambo za muda mrefu kuwa Yanga wataifunga Azam ambayo wao kwao imekuwa sio kazi na wamediriki kutoa baadhi ya misemo kuwa Azam watabaki kuwa Bidhaa bora na wao Yanga kuwa ni timu bora, sasa hapo jana tarehe 22/09/2013 mambo yaliwageukia hao Timu bora na wakajikuta wakichapwa bao 3 kwa 2 na hao wanaowaita bidhaa bora.

Mambo yalianza kwa Azam kujipatia bao la kuongoza kupitia kwa John Boko 'Adebayo' ambae amekuwa akiwafunga mara nyingi katika dikika ya kwanza tu ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kabisa kutoka kwa Mganda Brian Umony ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Yanga wakitafuta nao bao la mapema ili kuwapoteza Azam na juhudi zao zilizaa matunda pale walipopata bao la kusawazisha kupitia kwa Didier Kavumbagu na baadae kuongeza bao la pili kupitia kwa Hamis Kiiza 'Diego' aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Gerison Tegete ambae jana hakuwa makini kwani alikosa mabao mawili tena ya wazi.

Azam walijipatia bao la pili kwa njia ya Tuta baada ya beki mmoja wa Yanga kuunawa mpira ndani ya Eneo la hatari na Mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo iliwekwa kimiani na Mchezaji mwenye kasi, nguvu na akili nyingi Kipre Herman Chetche akitokea Bench huku Ali Mustafa 'Bartez' wa Yanga akienda kulia na mpira kelekea kushoto kwake.

Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kuonesha kandanda safi kwa mchezo wao wa kasi na pasi ndefu ndefu ambazo ziliisumbua sana ngome ya Azam lakini juhudi zao hizo zilikwamishwa na Mchezaji Chipukizi Faridi Musa baada ya kupokea pasi safi kutoka wingi ya kulia kwa Kipre Chetche aliyewakimbiza mabeki wa Yanga na kutoa pasi ya Banana Chop kwa mfungaji ambae bila ajizi akamwita Ali Mustafa na Kumfunga kwa guu lake la kushoto na kuipa Timu yake bao la 3 na la ushindi ambalo liliwakatisha tamaa kabisa Yanga kwakuwa muda ulikuwa umekwisha kabisa.

Tazama Picha za Mchezo huo hapa chini kwa hisani ya BIN ZUBEIRY:
 David Charles Luhende akimfanyia madhambi Kipre Chetche
 Kevin Yondani akiokoa kwa kichwa na mpira wa Brian Omony ukamkuta John Bocco akaukwamisha nyavuni na kuipatia Azam bao la kwanza.
 Farid Mussa akimtoka Beki wa Yanga Mbuyu Twite.
 John Bocco akijiandaa kumtoka Twite.
 Joackins Atudo wa Azam akiwania mpira mbele ya Simon Msuva wa Yanga
 Simon Msuva wa Yanga akimtoka Waziri Salum wa Azam
 Athumani Iddi 'Chuji' akimtoka Farid Mussa wa Azam
 Azam FC wakishangilia bao la pili la kusawazisha baada ya penati iliyopigwa na Chetche.








Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU