Facebook Comments Box

Friday, June 28, 2013

BARACK OBAMA KUPEWA PHD YA HESHIMA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

Taarifa ambazo zinasikika zikimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zinasema ya kuwa Ocean Road itabadilishwa jina lake na kuitwa, "Barack Obama Avenue" kwa heshima ya Rais huyo wa 44 wa taifa la Marekani.

Taarifa nyingine zinasema kuwa Obama pia atatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima na Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT) kwa kutambua mchango wake katika maisha ya binadamu kwenye nyanja ya maendeleo ya kiuchumi.

Amenukuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwete akisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Rais Obama anatunukiwa tuzo hiyo akitanguliwa na hayati Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela na Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

OUT imeshatoa pia shahada za heshima kwa mtafiti na mtetezi wa Sokwe wa Gombe, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano bwana David Mellor.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU