Facebook Comments Box

Friday, June 28, 2013

NDEGE ZA MAREKANI ZAWASILI DAR ES SALAAM


DAR ES SALAAM.   MAKACHERO wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatar ajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.
Meli za kivita na ndege ya kijeshi
Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.
“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU