Facebook Comments Box

Thursday, May 9, 2013

SAKATA LA BOMU KANISANI: SERIKALI YA SAUDI ARABIA YASEMA RAIA WAKE WAMEKAMATWA KIMAKOSA

Serikali za Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE) zimezungumzia kukamatwa kwa raia wake, ambao wanahusishwa na tuhuma za kurushwa kwa bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Viongozi wa Serikali walikaririwa wakisema wageni waliokamatwa raia watatu ni wa Saudi Arabia na mmoja wa UAE ambao walikamatwa wakati wakiondoka nchini kupitia Namanga.
Balozi wa Saudi Arabia
Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Momina alikaririwa na mashirika ya habari ya kimataifa akikiri kukamatwa kwa raia wa nchi yake na kusisitiza kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumhusisha na shambulizi hilo kwani alikuja Tanzania kutalii.
Momina alisema alikutana na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kinachochunguza suala hilo kwenye kituo cha polisi anaposhikiwa raia wake akitaka kujua kama mtu wao amewekwa vizuri.
“Tuna matumaini makubwa kuwa wataachiwa na tutaendelea kufuatilia suala lao hadi tuone mwisho wake,” alisema Balozi huyo na kusisitiza kwamba hawaondoki Arusha.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya UAE, kupitia mtandao wa Twitter ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu suala la raia wake watatu waliokamatwa. Ilisema walikuwa wanafanya kazi kwa karibu na ubalozi wa nchi yao huko Tanzania ili kufahamu hatima ya watu wao.
UAE imesema inapinga kwa nguvu zote vitendo vya ugaidi na iko tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania juu ya raia wake kuhusishwa na tukio hilo.
Na afisa mkubwa wa serikali ya Abu Dhabi anasema raia wake walikamatwa kimakosa na amesema mamlaka ya UAE wamepokea ripoti kutoka kwa wanaochunguza tukio hilo kuwa hamna uhusiano kati ya ulipuwaji wa bomu hilo na raia wake hao walio kamatwa. Na aliongeza kuwa wanasubiri raia wao waachiwe ili waweze kuwapokea nchini kwao.
 Sourse: GULF NEWS


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU