Facebook Comments Box

Friday, February 8, 2013

DKT. GHARIB BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MAREKANI




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, Feb 6, 2013.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU