Facebook Comments Box

Tuesday, April 9, 2013

BAADA YA KUIPA STARZ USHINDI WA BAO 3 KWA 1 DHIDI YA MOROCO SAMATA ATEGEMEWA KUIUA BOTSWANA JUMAPILI



TP Mazembe watawakaribisha Mochudi Centre Chiefs jijini Lubumbashi Jumapili huku macho yote yakiwa kwa mshambuliaji Mbwana Samata kuwavusha kuingia raundi ya pili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Samata amereja Mazembe akiwa na ari kubwa baada ya kufunga mabao mawili kwa Taifa Stars iliyoshinda 3-1 nyumbani dhidi ya Morocco jijini Dar-es-Salaam katika mchezo wa kusaka kufuzu kushiriki Fainali za  Kombe la Dunia 2014.
 
Kiwango chake kimekuwa ni habari njema kwa kocha wa Mazembe, Lamine Ndiaye mwenye matumaini ya kuiongoza timu hiyo ya DR Congo kuibwaga Mochudi katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Mazembe kwa sasa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Mochudi ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 16 jijini Gaborone, ambapo goli hilo pekee lilifungwa na Samata.
 
Pamoja na ukweli kwamba ubora wa Mazembe unamtegemea Samata, kocha wa Mochudi, Madinda Ndlovu bado anaamini kuwa kikosi chake kitafanya maajabu Lubumbashi hapo Jumapili.
 
"Bado hatujakata tamaa pamoja na kuwa tumefunga bao moja nyumbani kwetu,” alisema Ndlovu.
Wakati huo huo; hakuna timu iliyowahi kuifunga Mazembe jijini Lubumbashi kwa zaidi ya miaka kumi sasa katika mashindano haya ya Afrika.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU