Ukuta
ambao unatenganisha studio za Shirika la Taifa la Utangazaji, TBC,
Makao Makuu na barabara ya Nyerere umebomolewa kwenye upande wa barabara
ya Mandela inayoelekea Bandarini.
Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana na wafanyakazi wa ofisi hizo wamedai kuwa hawakuwa na taarifa yoyote, wala alama maafufu ya “X” ambayo huwa inaashiria kuwa eneo hilo litabomolewa wakati wowote.
Ukuta huo ulivunjwa mchana wa leo kwa mfululizo kuanzia maeneo ya mataa ya TAZARA.
Mshana alisema kuwa kwa unyeti wa kituo hicho na mali zake za thamani, ambacho pia ni mali ya Wananchi na Serikali, haikupaswa ukuta wake kuvunjwa kiholela na kuacha eneo hilo likiwa wazi.
Watu waliokuwa eneo la jirani walijizolea na kuondoka na nondo zilizotokana na kuvunjwa kwa ukuta huo.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog