Facebook Comments Box

Saturday, February 16, 2013

UMOJA WA MATAIFA WASEMA MAZUNGUMZO NDIO NJIA SAHIHI YA KUMALIZA MIGOGORO YA KIDINI

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson
Wakati viongozi wakuu  mbalimbali nchini Tanzania  wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa
madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa
nao kwa upande wake  unaeleza kwamba ni
kwa  njia ya  mazungumzo 
migogoro ya dini inaweza kuepukika.

 Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa,  umetolewa na  Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa  chombo hicho ya kimataifa ,  wakati wa 
tukio maalum  la Muungano  kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia
ya  maelewano ya  madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika
mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha  wawakilishi kutoka  dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali
na mabalozi.

“Migogoro mingi inayoendelea  hivi sasa duniani,  ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya
imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii.  Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya
mazungumzo   ili kujenga maelewano   na
kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema  Naibu Katibu Mkuu

Na kuongeza kuwa, dini zote
zimekuwa  mstari wa mbele katika juhudi
si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya  kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma  kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.

 Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za  kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu
na  mateso  katika jamii.

Na kwa sababu hiyo akasisitiza
kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali  kuharibu na kuvuruga amani  na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na
madhehebu ya dini .



 “Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu
wenye misimamo mikali  kuharibu kazi
nzuri zinazofanywa na  jumuia za kidini
kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson

Akaelezea  wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa  na vikundi vyenye misimamo mikali
kueneza  kampeni za chuki na  vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu
ili wao watimize malengo yao.

“Kwa kawaida  vijana wana nguvu.  Tunapashwa 
kutafuta   njia nzuri na sahihi za
kuwafanya wazitumie nvugu  zao kuboresha
maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Naye 
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa  upande wake alisema  Umoja wa Mataifa unaweza  kufaidika sana  kama viongozi wote wa dini watajihusisha na
kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka  Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na
madhehebu ya dini.

“ Hebu basi  na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani
zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana
wenyewe kwa  wenyewe,ikiwa  ni pamoja na 
uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti
zetu za imani”.

Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila
mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya
kwamba kama vyanzo vilivyopita  vya
migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya
kuitumbukiza dunia katika  machafuko ya
kutisha.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU