Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea 
katika mkutano na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana
 na Tume kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya  katika ukumbi wa 
Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry 
Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya Mamlaka hiyo 
kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa 
Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti 
wake Jaji Joseph Warioba (wa sita kutoka kushoto) katika picha ya pamoja
 na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliongozwa na 
Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne kutoka kushoto) 
mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya 
jijini Dar es Salaam.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
