Facebook Comments Box

Thursday, October 24, 2013

UHABA WA MBAO KUPATIKANA BAADA YA MSITU UNAOTEGEMEWA WA SAO HILL KUTEKETEA KWA MOTO


 Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa  umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka katika msitu huo.
 Askari polisi akimamisha  msafara  wa rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili na la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa  yamesimama
 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito  ulitanda barabarani


 Msafara  ukipita  eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto  huo


Yakiwa ni masaa takribani mawili  kupita  kutoka Rais Jakaya  Kikwete kufanya  kikao chake  cha majumuisho   ya ziara  yake   na  viongozi wa mkoa wa Njombe na  kuwataka  kuchukua hatua  katika kuthibiti moto  ili  kuepusha ukame ,moto  mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa  wa Sao Hill Mufindi na kupelekea  msafara  wa  Rais kusimama kwa  muda  kiusalama kutoka na moshi mzito  uliotanda  barabara  kuu ya Iringa Mbeya .

Moto  ulio ulioanza  kuwaka  mida ya saa nane  mchana    ulizuia kwa  muda  kama dakika tatu hivi msafara  wa Rais Kikwete  kufimama katika eneo la Changalawe mjini  Mafinga umbali  wa mita 2  kufika  njiapanda  ya   kuingia ofisi ya mkuu  wa wilaya ya  Mufindi na Ikulu ndogo  ya  wilaya ya Mufindi.

Kutokana na tukio hilo la moto msafara  wa rais  Kikwete  ulisimama na baada ya maofisa  usalama  kushuka na kutazama usalama  zaidi wa msafara  huo ndipo  walioruhusu msafara  huo  kuendelea .

Hata  hivyo  jitihada  kubwa  zilionekana kufanywa na  kikosi  cha askari  wa  JKT Mafinga  pamoja na  wananchi ambao  walikuwa  wakizima  moto  huo .

Huku   vyombo  vya  usafiri  yakiwemo mabasi ya abiria yanayosafiri  kutoka Dar es Salaam kuwenda  mikoa ya  kusini na nchi  za kusini mwa Tanzania yakikwama  kuendelea na  safari  kutoka na moto  huo kushikakasi na  moshi  mzito  kutanda  barabara 

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  alisema kuwa  uongozi  wa  mkoa  tayari  umeagiza  mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka   waliohusika na  uchomaji  moto huo ili  kuchukulia  hatua  kali.


Mkuu  huyo  wa  mkoa alisema  kuwa mkoa  wa Iringa umekuwa  ukichukua hatua  kali  kwa wale wote wanaoanzisha  moto  kichaa kama  huo hivyo  kupitia  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika  watasakwa  popote  walipo .

Mbali na  hilo mkuu  huyo amelipongeza  jeshi la JTK Mafinga kwa  kuchukua hatua  za haraka katika kukabiliana na moto  huo huku akisema madhara  zaidi  yatokanayo na moto  huo yatatolewa baada ya  moto  huo kuthibitiwa Chanzo: Francis Godwin-Iringa


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU