Hii ndiyo ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo tu ya hizo kilometa tatu.
Meya Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao.
Picha zifuatazo ni za siku Meya Silaa alipotembelea ujenzi.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Ukonga Moshi Bar ya kilometa 3 kwa kiwango cha changarawe awamu ya kwanza, ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinu uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha. Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi millioni 90. Pesa za ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Pia barabara hiyo itawekwa lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-Mazizini kulekea Moshi Bar
Mwonekano wa barabara hiyo

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog