Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi
amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa shirikisho la soka nchini, TFF.
Malinzi ameshinda uchaguzi huo wa leo uliokuwa ukifanyika kwenye ukumbi
wa Mikutano wa NSSF, Water Front jijini Dar es Salaam kwa kupata
asilimia 78 ya kura na kumbwaga mpinzani wake Athuman Nyamlani.
Malinzi
atachukua nafasi ya Leodegar Tenga aliyekuwa Rais wa TFF tangu mwaka 2005.
Taarifa za kuchaguliwa kwa Malinzi kuwa rais mpya wa TFF, zimepokelewa
kwa furaha na binti yake, mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva
aliyetweet:
My dad is the new president TFF¦.. What a good news. Cant wait to
get home and give him a big hug and a kiss. Gooooo Daddy” Diva (@DivaBos) October 27, 2013
Malinzi alishika nyadhifa mbalimbali Yanga zikiwemo seneta, mkurugenzi wa kuchaguliwa, kaimu katibu mtendaji na katibu mkuu.
Amekuwa mwenyekiti wa mashindano ya mpira wa miguu mkoa wa
Pwani (2009-2011) na mjumbe wa Baraza la Michezo la Mkoa wa Dar es
Salaam (2009-2012).
Toka 2011 hadi sasa ni mjumbe kwenye Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Mpira wa Miguu wilaya ya Misenyi, pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama
cha Mpira wa Miguu mkoa wa Kagera.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog