Facebook Comments Box

Tuesday, October 15, 2013

HUKUMU YA BABU SEYA KUFANYIWA MAPITIO UPYA NA MAJAJI WATATU

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania waliotoa hukumu ya wanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking “Babu Seya” na mwanaye Johnson Nguza “Papii Kocha”, linatarajia kupitia upya hukumu hapo Oktoba 30, mwaka huu, gazeti la HabariLeo limeandika.

Nguza Viking na wanaye watatu walihukumiwa na Hakimu Mkazi  Addy Lyamuya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kifungo
cha maisha jela mwaka 2004.

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa mwezi Februari, mwaka 2010 katikaMahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam lakiniJaji Thomas Mihayo naye aliwatia hatiani na kuafiki hukumu ya Mahakama ya Kisutu.

Walikata tena rufaa katika Mahakama ya Rufani na safari hii, Jopo la majaji watatu -- Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati -- liliwaachia huru Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika hawakuwa na hatia, na kuamuru Nguza Viking na Johnson Nguza watumikie kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya Msingi kama ilivyohukumiwa na mahakama zilizotangulia.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU