Facebook Comments Box

Tuesday, October 15, 2013

'IYD AL-ADHW-HAA AL-MUBAARAK - TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM

Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh



Kwa Munaasabah huu wa furaha wa siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Adhw-haa tunapenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd).

Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu. Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku. Ndugu zetu Waislam walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko pote walipo Waislamu ulimwenguni.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn.

kwenye picha ifuatayo ni Takbiyrah ya 'Iyd

Tunapenda kuwakumbusha kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyratul Muqayyid ambayo ni Takbiyrah inayotakiwa kusomwa kila baada ya Swalah za fardhi kuanzia siku ya 'Arafah baada ya Swalaatul-Fajr hadi mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Aswr ndio kumalizika kwake. 

Na inapasa kuwakumbusha ndugu wengine ili kila mmoja apate thawabu za kuifufua Sunnah hii ambayo wengi wameiacha. Thawabu hizo zitazidi kuongozeka kwa yule atakayeanza kumfunza mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kutekelezwa na kuenezwa: Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
  ((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً .... )) أخرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao chochote…)) [Muslim]
Inavyopasa kufanya Takbiyrah baada ya kutoa salaam ni kama ifuatavyo:
  الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد
"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar WaliLLaahil-hamd


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU