Facebook Comments Box

Tuesday, September 24, 2013

HUYU NDIE MTU MWEUSI NA MUISLAM WA KWANZA KUWA MBUNGE UJERUMANI



Diaby Karamba mwenye umri wa miaka 51, mzaliwa wa Senegal amekuwa muislamu mweusi wa kwanza kuchaguliwa katika Bunge la Ujerumani kutoka chama cha Social Party.
Karibu moja ya Tano ya watu wa Ujerumani milioni 80 ni wahamiaji au watoto au wajukuu wa wahamiaji ambapo wachache wameshaingia katika Bunge la Shirikisho.Kabla ya kuchaguliwa Diaby Karamba, hapakuwahi katika historia ya Ujerumani kuwa na mbunge mweusi, licha ya watu zaidi ya 500,000 wa asili ya Afrika inaaaminika wanaishi Ujerumani.
“Uchaguzi wangu ndani ya Bunge la Ujerumani ni wa muhimu na kihistoria,” alisema Diaby ambaye alihamia Mji wa Halle mwaka 1986 baada ya kupata udhamini wa kusoma Iliyokuwa nchi ya Ujerumani Mashariki. Diaby ambaye alipata uraia wa Ujerumani mwaka 2001, alisema kipaumbele chake itakuwa ni kukuza fursa sawa katiak elimu. “Kila mtoto aliyezaliwa nchini Ujerumani inapaswa kuwa na nafasi ya kuwa na mafanikio katika shule bila ya kujali historia yao ya kijamii au mapato ya wazazi wao,” alisema
Zaidi ya Dazeni ya wahamiaji walichaguliwa katika uchaguzi wa Jumapili .Wengi walipitia chama cha Social Democratic na chama cha mazingira cha Green Party. Muislamu mwingine Giousouf Cemile mwenye umri wa miaka 35, alichaguliwa katika mji wa Magharibi wa Hagen. Giousouf Cemile alizaliwa Ujerumani na wazazi wake wote wana asili ya Uturuki.
Wabunge kadhaa wenye asili ya Kituruki wamewahi kuchaguli katika siku za nyuma. Katika viti 630, asilimia 5.4 wanatoka familia za wahamiaji.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU