Klabu ya Arsenal iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitoa kwa matuta West Brom Uwanja wa The Hawthorns na kuingia Raundi ya Nne ya michuano hiyo. Eisfeld aliifungia Arsenal dakika ya 61 kabla ya Berahino kusawazisha dakika ya 71.
Arsenal itamenyana na wapinzani wao katika Jiji la London, Chelsea 
katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup 
baada ya kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
Mechi
 hiyo iliisha kwa sare ya 1-1 usiku wa jana ndipo ilipoamuriwa zipigwe penati ambapo Washindi walipata penati zao 4 na walikosa moja wakati Westbrom wao walikosa penati mbili. 
 
 Nacho Monreal akiifungia Arsenal penalti ya ushindi

Monreal na wachezaji wenzake wa Arsenalwakishangilia
Arsene Wenger akizungumza na Nicklas Bendtner kabla ya kupiga penalti yake

Thomas Eisfeld akiifungia bao la kwanza Arsenal

Nicklas Bendtner alikuwa mwiba usiku wa jana The Hawthorns

Mdenmark Nicklas Bendtner amekuja kwa staili ya nywele za David Beckham

Bendtner na Eisfeld wakipongezwa na wachezaji wenzao
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog