Ridhiwani Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa eneo la Mafia |
Katika kamati hiyo ambayo
Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe
atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa
mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana
na mahitaji kwa kipindi hicho.
Mara baada ya kutambulishwa kwa
wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa
mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na
kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo
unafanikiwa.
"Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza
kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika
ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo
litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani
Aidha
Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda
mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili
kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa
sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.
Ridhiwani mwisho
alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu
bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga
sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo
yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog