Facebook Comments Box

Thursday, March 21, 2013

KESI YA PONDA YAFUFUA MAZITO

 
KESI inayomkabili Katibu wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, imezidi kuibua mambo mazito, ambapo safari hii, waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume wametajwa katika kesi hiyo.
 Shahidi wa upande wa utetezi, Bilali Wakera (87), mkazi wa Mkoa wa Tabora, ambaye ni kiongozi wa dini alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Nyerere na Karume walichangia kudidimiza Uislamu.
Akiongozwa na Wakili Juma Nassoro, Wakera alidai kuwa miaka ya nyuma Waislamu walikuwa dhoofu kwani walikuwa viongozi wawili, Aga khan ambaye alikuwa ni kiongozi wa dunia na Rais wa Misri Nassar walichukua dhamana ya kuwasaidia Waislamu.
Viongozi hao walianzisha East Africa Muslim Welfare Society kama chombo cha kuwasaidia Waislamu wote. Alidai kuwa chombo hicho kilikuwa na mali nyingi, vikiwemo viwanja na kimojawapo kilikuwa ni Kiwanja cha Markaz Chang’ombe. Alidai kuwa dhumuni la kiwanja hicho ilikuwa kujenga Chuo cha Kiislamu. Waikara alidai kiwanja hicho kilitakiwa kijengwe chuo cha ghorofa tatu, lakini anashangaa kilichopo sasa kimejengwa ghorofa moja.
 Hata hivyo, alidai kuwa kwa sababu yeye alikuwa ni kiongozi mkubwa katika chombo hicho, Hayati Mwalimu Nyerere alimwita na kumwambia aachane na mambo hayo kwanza hadi wapate uhuru. Shahidi huyo alidai kuwa Nyerere alimuahidi kuwa watakapopata uhuru atawasaidia Waislamu, lakini hakutekeleza ahadi hiyo.
Alidai kuwa baada ya Nyerere kutotimiza ahadi hiyo aliwaeleza Waislamu kuwa yeye aliwekeana ahadi na Mwalimu, lakini hakuitekeleza ndipo walipoanza kukwanguana na Mwalimu Nyerere.
 Pia alidai kuwa Karume aliwapatia fedha watu wake wazisambaze mikoani ili kuvunja chombo hicho na kwamba walitembelea mikoa 20. Mikoa 12 walikataa chombo hicho kisivunjwe na mikoa iliyobaki walikubali kivunjwe. ”Hata mimi nililetewa sh. 40,000 na Adamu Nasibu, lakini nilizitaa kwa sababu nilikuwa nakitetea chombo cha Waislamu,” alidai Waikera.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU